Cristiano Ronaldo kurudi Madrid kuwavunja moyo Atletico

0

Mshambulizi huyo aliyekuwa akichezea Real Madrid amefunga mabao 22 katika mechi 31 ambazo amecheza dhidi ya Atletico Madrid na anatarajiwa kundeleza mtindo huo akiwa kwenye jazi ya Juventus leo usiku watakapokutana katika awamu ya kwanza ya raondi ya 16 klabu bingwa barani Uropa.

Ronaldo alipewa kadi nyekundu katika mechi yake ya kwanza ya klabu bingwa barani Uropa akiichezea Juventus baada ya kucheza dakika 28 dhidi ya Valencia. Juve hata hivyo walishinda mechi hiyo 2-0.

Juventus wanatarajia kwamba Ronaldo waliyemnunua kwa € 100 milioni atawasaidia kupata ushindi dhidi ya Atletico ikizingatiwa kuwa yuko na rekodi nzuri dhidi yao na vile vile ndiye anayeongoza kwa wafungaji bora kwenye Serie A ya Italia kwa mabao 19 na assist 8 kufikia sasa.

”Tuko sawasawa kwa sasa, licha ya Parma kutusumbua bado tuko sawa,” alisema Allegri. Alizidi kueleza kuwa Chiellini na Bonucci wako sawa kushiriki mechi hiyo baada ya kutoka kwa majeraha. Kabla ya kujiunga nao, Ronaldo alikuwa amefunga mabao 10 kwa mikutano 7 dhidi ya Juve na kwa sasa wako na nafuu atakuwa upande wao.

Ronaldo amewavunja moyo kwenye fainali za Copa del Rey na klabu bingwa barani Uropa. Mjini Lisbon, Ronaldo alifunga bao la nne kupitia penalti dhidi ya Atletico, Real wakishinda 4-1. Nusu fainali ya 2016/17, Ronaldo alifunga hat-trick katika awamu ya kwanza na kuwasaidia Real kuwabandua Atletico na amefunga mabao za kuhesabika dhidi yao kwenye Laliga.

Loading...

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More