Liverpool vs Arsenal, Uchambuzi na Ubashiri

0

Liverpool na Arsenal watakabiliana siku ya Jumamosi tarehe 24 Agosti mwaka huu ugani Anfield. The reds na the gooners wanaongoza jedwali la premier league, wakishikilia nafasi ya kwanza na pili mtawalia, wote wakiwa na alama 6 baada ya kushinda mechi zao mbili za ufnguzi ila the reds wana ubora wa mabao.

Liverpool hawajashindwa mechi za premier league 39 za mwisho walizocheza nyumbani. Pia, wamefnga mabao 2 au zaidi katika mechi zao za mwisho 11 za ligi.

Arsenal hawajashindwa kwenye mechi zao 5 za mwisho walizocheza kwenye premier league. Ikumbukwe kuwa Arsenal hawajapata ushindi dhidi ya Liverpool katika mechi 6 za mwisho walizokabiliana nao.

Mechi 6 za mwisho ambazo timu hizi zimekutana, 5 kati yao imeshuhudia mabao 4 au zaidi huk kila timu ikipata bao katika mechi 5 kati ya 6 za mwisho walizocheza kwenye kabiliano hili.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa Disemba 29 mwaka jana ambapo Liverpool walipata ushindi ya mabao 5-1.

Loading...

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More