Piga kura kwa mchezaji bora wa mwezi, Premier League

0

Jumla ya wachezaji wanne wameteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora mwezi wa kwanza msimu huu kwenye premier league. Sergio Aguero wa Manchester City, Ashley Barnes wa Burnley, Debruyne wa Man City, Firmino na Pukki wa Liverpool na Norwich mtawalia, ndio wachezaji ambao wameteuliwa kupigiwa kura.

Teemu Pukki amezungumziwa sana baada ya kufunga mabao katika mechi zake 3 za kwanza msimu huu. Tayari amefunga dhidi ya Liverpool, Chelsea na Newcastle.

Aguero amefunga mabao 6 na ndiye mfungaji bora kwa sasa kwenye premier league. Barnes amefunga mabao manne huku De Bruyne akisifiwa sana kutokana na usaidizi wake kuzalisha mabao (assists) mara nyingi.

Firmino amekuwa na msimu bora huku akifunga mabao 2 na assists 2. Pukki na Sterling wote wamenawiri pia huku wakiwa na mabao 5 kila mmoja msimu huu.

Sterling alifunga hat-trick ya kwanza kwenye premier league tangu Drogba, 2010 na pia alifunga dhidi ya Tottenham na Bournmouth. Upigaji kura unamalizika siku ya Jumatatu tarehe 9 Septemba 2019, saa mbili usiku masaa za Afrika Mashariki.

Unaweza kupiga kura kupitia hii link https://plpotm.easports.com/?utm_source=www.premierleague.com&utm_campaign=website&utm_medium=link

Loading...

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More