Jiraha la De Gea Lathibitishwa

0

Kocha wa Uhispania Robert Moreno amethibitisha kuwa mlinda lango wake David De Gea alijeruhiwa wakati wa makabiliano yao dhidi ya Sweden ambapo walimaliza sare ya bao 1-1.

Taarifa hizi ni pigo kubwa haswa kwa Manchester United ambao wanatarajiwa kumenyana na viongozi wa Premier League, Liverpool mnamo siku ya Jumapili 20 Oktoba 2019 ugani Old Trafford.

Liverpool hawajapata ushindi ugani Old Trafford katika safari zao tano za majuzi na Klopp atakuwa anatafuta ushindi wake wa kwanza dhidi ya Man United wanao shikilia nafasi ya 12 kwenye jedwali.
Mechi hiyo itachezwa saa kumi na mbili na nusu jioni masaa za Afrika Mashariki.

Loading...

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More